top of page

Kwaheri Mama Lucy Kibaki


Lucy Kibaki, Mwai Kibaki

Ninazitoa heshima zangu kwa Mama Lucy Kibaki aliyetuaga leo. Mama Lucy aliaga hospitalini mjini London alikopelekwa siku chache zilizopita ili kupata matibabu maalum. Mama Lucy alikuwa mke wa rais wa tatu wa Kenya, Mheshimiwa Mwai Kibaki.


Alikuwa mama wa taifa wa pili baada ya Kenya kupata uhuru mwaka 1963. Mama Ngina Kenyatta, mkewe Mzee Jomo Kenyatta alikuwa wa kwanza. Kwa miaka 24, chini ya utawala wa rais wa pili, Daniel Arap Moi, hakuna aliyeshikilia cheo hicho muhimu kwa vile Moi hakuwa na mke rasmi. Kwa nini? Ni ndefu.


Mama Lucy aliipa ofisi hiyo nguvu ya kipekee kutokana na vile alivyoshiriki katika mirada ya kuwasaidia walemavu, watoto, na akina mama. Kuna hospitali kubwa jijini Nairobi inayojulikana kama Mama Lucy, kutambua mchango wake mkubwa katika nyanja ya afya.


Aidha, Mama Lucy alisifika kwa kuitetea familia yake. Aliwacharaza makofi wanasiasa waliosemekana kulewa katika ikulu na kutomheshimu mumewe rais. Vilevile, alivamia ofisi za gazeti la Standard na kuleta vurugu kubwa iliposemekana kuwa gazeti hilo lilikusudia kuchapisha makala ya kashfa iliyoigusa familia yake. Vitendo hivi viwili vilimletea dhihaka kwa wengine na fahari kwa wale waliofikiria anailinda na kuitetea familia take.


Mama Lucy hakuonekana hadharani kwa miaka 5 na raia hawakujua ukweli kuhusu kilichomsumbua. Ingefaa viongozi wabadilishe mwenendo huu na kuwa na uwazi zaidi hata kuhusu masiala ya afya.

Mama Lucy atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa nchini Kenya. Aliweka msingi bora kwa Mama wa Taifa watakaomfuata na hata wanasiasa wanawake nchini Kenya. Ujasiri wake na moyo wa kujitolea ulidhihirisha kuwa kazi ya Mama wa Taifa kuandamana na raisi kwenye sherehe rasmi, kumpikia rais chajio kitamu na kuwapa wageni wa ikulu chai na biskuti.


Tunapomuaga, ninampa heshima zangu za kipekee na kuomba mola amlaze pema peponi.

Featured Posts
Recent Posts
Search By Tags
Follow Us
  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • Google Classic
bottom of page