top of page

Safari ya Cape Town




Alfajiri na mapema tarehe Juni 30 niliichukua Uber kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Safari ya kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini ilikuwa imewadia. Kongamano kuu la wanaisimu duniani lilikuwa limenialika niwasilishe utafiti wangu. Utafiti nilikuwa nimeufanya. Wasilisho lilikuwa tayari na tiketi mkononi. Nilikuwa na hamu kuiona nchi ya Mandela, Steve Biko, Winnie Mandela, na mashujaa wengine wa ukombozi. Sijawahi kuzuru sehemu ya kusini ya bara letu.


Mji wa Cape Town ulinishangaza nilipowasili. Tofauti za kirangi na kitabaka bado zinajidhihirisha baya

na. Haya kongamano likaisha na nikafurahi sana kukutana na wakwasi wengi wa isimu ambayo nimewasoma. Aidha nikakutana na marafiki na wasomi wenza ambao hatujaona kwa muda. Nikawa za siku moja na nusu ya matembezi kabla ya kurejea.


Kwanza nikaukwea mlima uitwao "Lion's Head." Nimekwea milima Lo

ngonot mara nyingi. Aidha Aberdares and Elgon nimeionja. Lakini huu ulikuwa na changamoto na hatari zake. Hata vivyo niliweza kufika kilele na kushuka salama. Miguu ilikuwa inawasi na kuinung'unikia. Chambilecho wahenga "kupanda mchongomano si neno, kushuka ndio ngoma."




Singeondoka Cape Town pasi na kufika maeneo mawili niliyoyasoma darasa la jiografia katika shule ya msingi na sekondari: Table Mountain na Cape Point. Kwa bahati, Mlima wa Meza upo jirani ya Lion's Head. Nichakua Uber hadi lango ya kuingia. Nikafika kilele na kut

ambua kilele cha mlima kwa kweli ni kama meza. Umaridadi wa mazingira katika sehemu hii ya Afrika - milima, bahari, na visiwa - kwa kweli ulichangia pakubwa ukoloni na ukatili wa walowezi ambao hawatuka kuondekea uzuri huu wote licha ya kuwa ilikuwa ardhi ya Afrika na Waafrika. Ndiyo maana wakamfungia Nelson Mandela na wanaharaki wengi miaka yote gerezani na kuwaua wazalendo wengi kama Steve Biko.



Featured Posts
Recent Posts
Search By Tags
Follow Us
  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • Google Classic
bottom of page