top of page

Jumanne Kuu na Donge Nono

USA Presidential Election Primaries 2016

Haya! Wenye kunena wamenena! Yaani wapiga kura wamedhihirisha msisimko wao na mapendeleo yao katika ya wanasiasa wanaowania kitu cha urais nchini Amerika. Hillary Clinton na Donald Trump waliiubuka na ushindi mkubwa. Bernie sanders alijishindia majimbo manne naye Clinton akajishindia majimbo saba. Kwa upande wa wanarepublican, Marco Rubio alishinda jimbo la kwanza na la pekee kwenye mchujo huu. Ted Cruz akashinda matatu na kupata jumla ya manne kufikia sasa. Mengineo akayafagia Trump.

Ushindi wa Trump unaendelea kuwapa kiwewe vigogo wa chama chake ambao hawampendi na hawana uwezo wa kumdhibiti. Kwa vile anatumia utajiri wake kugharamia uchaguzi wake, chama hakiwezi kumtisha kuwa hatapata msaada wa kifedha asipofuata mwelekeo wa chama. Hii ni mojawapo wa sifa zinazowafuatia wapiga kura wengi kwa vile hali ya siasa imezorota sana nchini humu. Imekabiliwa na ufisadi mkubwa na kura za maoni za mara kwa mara zinaonyesha raia wanaipendelea bunge la Congress kwa asilimia 19 tu. Yumkini wabunge na maseneta hawawakilishi wapiga kura bali wadhamini wao wenye donge nono. Kwa mfano, makampuni yenye kuuza mafuta, wauza bunduki, makampuni ya bima na mabenki makuu yanayoendelea kuwanyonya raia. Bernie Sanders pia anapata wafuasi wengi hasa wale wanaoamini pia kuhusu ufisadi huu wa kisiasa.

Si ajabu kuwa nchi tajiri kama Marekani ina wengi wa raia na watoto wanaolala njaa, hawana mahitaji muhimu, miundombinu inaendelea kuzorota, na hali ya maisha ya wengi imedidimia. Lakini kwa upande wa pili wapo wale wachache wanaoishi maisha ya kistarehe ajabu.

Tags:

Featured Posts
Recent Posts
Search By Tags
Follow Us
  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • Google Classic
bottom of page