Kwaheri Mwaka 2020
- Mungai Mutonya
- Jan 3, 2021
- 1 min read
Updated: Jan 27, 2021

Tukomea mbali mwaka 2020
Rudi ulikotoka na balaa zako.
Umedhalilisha dunia kwa janga kuu
Umeleta maafa yasiyokadirika
Umewafungia watu majumba
Watoto hawawezi cheza nje na wenzao.
Hewa umeihatarisha na kutulazimishia barakoa.
Kazi zimefunguwa na biashara kufilisika.
Njaa imekithiri kwa pesa kupungua.
Lakini nashindwa tukulaumu mwaka 2020
Au tujilaumu sisi sote
kwa kudhalilisha mazingira yetu.
Kwa kutojali afya zetu
Kupapia pes na mali bila kujijali
Bila kujali wema na uhai wa mazingira yetu.
Ni rahisi kukulaumu 2020 lakini tujiangazie kurunzi kwanza.
Mwaka 2020 na kwa juhudi zetu
Tukaling'oa jitu la Marekani
kwa kura kochokocho kukatawaza
Hekima ya mzee Biden
Na ustadi wa dadetu Kamala.
Karibu 2021
Tuletee matumaini
Tuondolee janga hili
Tujikumbushe wajibu wetu duniani
Tuepushe maafa na uongozi mbaya.
Comments