top of page

Kwaheri Mwaka 2016

Updated: Nov 28, 2020


Gwen Ifill

Tuseme nini 2016?

Kwaheri, kwaheri, na kwaheri kabisa.

Nenda jumba la historia, ulale.

Tulikukaribisha kwa shangwe na matumaini.

Furaha, ufanisi, na amani tukatumaini.

Lakini ukatuletea maafa Syria,

Vurugu Sudan Kusini

Ugaidi Ulaya mzozo Libya,

Ingawa Colombia amani ilibisha hodi.

Kisiasa ulitubabaisha tosha.

Trump ulimtoa wapi?

Rodrigo Duerte wa Ufilipino naye?

Brexit nayo?

Na Putin kampa nguvu ja stereoids.

Muhammad Ali na Fidel Castro

Buriani 2016.

Buriani Bingwa Muhammad Ali

Buriani Fidel Castro

Buriani wanamuziki Prince na George Michael

Buriani mwanahabari Gwen Ifill

Karibu mwaka 2017

Tuletee amani

Twaomba furaha

Karibu mwaka mpya

 
 
 

Comentarios


Featured Posts
Recent Posts
Search By Tags
Follow Us
  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • Google Classic

FOLLOW ME

  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • c-youtube

© 2023 by Samanta Jonse. Proudly created with Wix.com

bottom of page