top of page

Hongera Mama Taifa na Wakenya


Beyond Zero Mobile Clinic

Maelfu kwa maelfu ya wakenya walijitokeza kushiriki kwenye mbio za nusu marathoni jijini Nairobi. Mbio hizi zilianzishwa na Mama wa Taifa, Bi. Margaret Kenyatta, kama njia mojawapo ya kuchangisha pesa za kampeni yake ya Beyond Zero.

Kampeni hii inalenga kununua kliniki zinazoweza kusafirishwa kutoka eneo moja hadi lingine ili kuwahudumia watoto na akina mama kwenye sehemu ambazo hazina huduma ya afya tosha. Itakumbukwa kwamba watoto wengi, mama wajawazito, na hata raia wengi hufa kutokana na shida za kiafya zinazoweza kuzuiwa. Ndiposa Mama taifa akajitolea kuongoza mradi huu. Amewahi kukimbia marathoni mjini London kuhamasisha watu kuhusu kampeni hii muhimu. Aidha amewajumlisha Mama wa Taifa wengine barani Afrika kutilia maanani afya ya akina mama na watoto. Si ajabu kwenye mbio za leo, Bi. Janet Kagame, Mama wa Taifa nchini Rwanda na mkewe Rais Kagame alikuja Nairobi kushiriki mbio hizi.

Margaret Kenyatta, Rachel Ruto, Janet Kagame running in Nairobi

Katika mwaka wake wa tatu, kampeni hii imeweza kununua kliniki 36 na kuzikabidhi kaunti nyingi za Kenya zenye haja ya huduma hii ya afya. Bi. Kenyatta anawapa wengi motisha kuona kuwa licha ya Bi Kenyatta ni mama wa miaka zaidi ya hamsini mwenye watoto wanne wakubwa anafanya mazoezi na kukimbia mbio hizi ndefu. Kuona kuwa zaidi ya watu 70,000 walijiandikisha kushiriki mbio hizi jijini Nairobi ni dhihirisho kuwa mfano wake wa kuboresha mwili kwa kufanya mazoezi unawapa motisha wakenya wengi. Pia moyo huo wa kujitolea ni mfano wa kuvutia moyo kwenye taifa ambalo linajitumbuiza kila siku na kila saa kwenye pipa la takataka ya siasa mbovu.


Mbio hizi zilisaidia kuchangisha zaidi ya shilingi 150 milioni zitakazotumika kuendeleza afya bora na pia kukabiliana na Ukimwi. Hongera sana, Mama Taifa, Bi Magaret Kenyatta. Hongera sana Makamu wa Rais na Mkeo kwa kushiriki. Hongera sana Janet Kagame. Hongera ndugu Wakenya kwa kujitolea na kuonyesha mfano mwema kwa ulimwengu. NINAJIVUNIA KUWA MKENYA.

 
 
 

Comments


Featured Posts
Recent Posts
Search By Tags
Follow Us
  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • Google Classic

FOLLOW ME

  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • c-youtube

© 2023 by Samanta Jonse. Proudly created with Wix.com

bottom of page